Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 11:11-24 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Mji hufanikishwa kwa baraka za wanyofu,lakini huangamizwa kwa mdomo wa waovu.

12. Anayemdharau jirani yake hana akili,mtu mwenye busara hukaa kimya.

13. Apitapitaye akichongea hutoa siri,lakini anayeaminika rohoni huficha siri.

14. Pasipo na uongozi taifa huanguka,penye washauri wengi pana usalama.

15. Anayemdhamini mgeni atakuja juta,lakini anayechukia mambo ya dhamana yu salama.

16. Mwanamke mwema huheshimiwa,mwanamume mwenye bidii hutajirika.

17. Mtu mkarimu hufaidika yeye mwenyewe,lakini mtu mkatili hujiumiza mwenyewe.

18. Faida anayopata mwovu ni ya uongo,lakini atendaye mema hakika atapata faida ya kweli.

19. Mtu anayepania kuwa mwadilifu ataishi,lakini anayechagua kutenda maovu atakufa.

20. Wenye nia mbaya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,lakini wenye mwenendo mwema ni furaha yake.

21. Hakika mwovu hataepa kuadhibiwa,lakini waadilifu wataokolewa.

22. Mwanamke mzuri asiye na akili,ni kama pete ya dhahabu puani mwa nguruwe.

23. Matazamio ya waadilifu yana matokeo mema;tamaa za waovu huishia katika ghadhabu.

24. Atoaye kwa ukarimu huzidi kutajirika;lakini bahili huzidi kudidimia katika umaskini.

Kusoma sura kamili Methali 11