Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 5:9-17 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Chakula chetu twapata kwa kuhatarisha maisha yetu,maana wauaji wanazurura huko mashambani.

10. Ngozi zetu zawaka moto kama tanurikwa sababu ya njaa inayotuchoma.

11. Wanawake wetu wanashikwa kwa nguvu mjini Siyoni,binti zetu katika vijiji vya Yuda.

12. Wakuu wetu wametungikwa kwa mikono yao;wazee wetu hawapewi heshima yoyote.

13. Vijana wanalazimishwa kusaga nafaka kwa mawe,wavulana wanayumbayumba kwa mizigo ya kuni.

14. Wazee wameacha kutoa mashauri yao,vijana wameacha kuimba.

15. Furaha ya mioyo yetu imetoweka,ngoma zetu zimegeuzwa kuwa ombolezo.

16. Fahari tuliyojivunia imetokomea.Ole wetu kwa kuwa tumetenda dhambi!

17. Kwa ajili hiyo tumeugua moyoni,kwa mambo hayo macho yetu yamefifia.

Kusoma sura kamili Maombolezo 5