Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 5:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ukumbuke ee Mwenyezi-Mungu, mambo yaliyotupata!Utuangalie, uone jinsi tulivyoaibishwa!

2. Nchi yetu imekabidhiwa wageni,nyumba zetu watu wengine.

3. Tumekuwa yatima, bila baba,mama zetu wameachwa kama wajane.

4. Maji yetu tunayapata kwa fedha,kuni zetu kwa kuzinunua.

5. Tunalazimishwa kufanya kazi kama punda,tumechoka lakini haturuhusiwi kupumzika.

6. Wamisri na Waashuru tumewanyoshea mikono,ili tupate chakula cha kutosha.

7. Wazee wetu walitenda dhambi na hawapo tena;nasi tunateseka kwa sababu ya makosa yao.

8. Watumwa ndio wanaotutawala,wala hakuna wa kutuokoa mikononi mwao.

9. Chakula chetu twapata kwa kuhatarisha maisha yetu,maana wauaji wanazurura huko mashambani.

10. Ngozi zetu zawaka moto kama tanurikwa sababu ya njaa inayotuchoma.

11. Wanawake wetu wanashikwa kwa nguvu mjini Siyoni,binti zetu katika vijiji vya Yuda.

12. Wakuu wetu wametungikwa kwa mikono yao;wazee wetu hawapewi heshima yoyote.

13. Vijana wanalazimishwa kusaga nafaka kwa mawe,wavulana wanayumbayumba kwa mizigo ya kuni.

Kusoma sura kamili Maombolezo 5