Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 2:13-22 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Nikuambie nini ee Yerusalemu?Nikulinganishe na nini?Nikufananishe na kitu ganiili niweze kukufariji,ee Siyoni uliye mzuri?Maafa yako ni mengi kama bahari.Ni nani awezaye kukuponya?

14. Manabii wako wamekuonea maono madanganyifu,hawakufichua wazi uovu wakoili wapate kukurekebisha,bali walikuonea kauli ya uongo na ya kupotosha.

15. Wapita njia wote wanakudhihaki;wanakuzomea, ee Yerusalemu,wakitikisa vichwa vyao kwa dharau na kusema:“Je, huu ndio ule mji uliofikia upeo wa uzuri,mji uliokuwa furaha ya dunia nzima?”

16. Maadui zako wote wanakuzomea,wanakufyonya na kukusagia meno,huku wakisema, “Tumemwangamiza!Kweli, siku ile tuliyoingojea kwa hamusasa imefika na tumeiona!”

17. Mwenyezi-Mungu amefanya yale aliyokusudia,ametekeleza yale aliyotishia;kama alivyopanga tangu kaleameangamiza bila huruma yoyote;amewafanya maadui wafurahie adhabu yako,amewakuza mashujaa wa maadui zako.

18. Kuta zako, ee mji wa Siyoni, zimlilie Mwenyezi-Mungu!Machozi na yatiririke kama mto mchana na usiku!Lia na kuomboleza bila kupumzika!

19. Usiku kucha uamkeamke ukalie.Mfungulie Mwenyezi-Mungu yaliyo moyoni mwako.Mwinulie mikono yako kuwaombea watoto wako,watoto wanaozirai kwa njaa popote barabarani.

20. Tazama ee Mwenyezi-Mungu uone!Je, kuna yeyote uliyemtendea ulivyotutendea sisi?Je, hata kina mama wawale watoto wao?Je, nao makuhani wauawe hekaluni mwako?

21. Maiti za vijana na wazee zimelala vumbini barabarani,wasichana na wavulana wangu wameuawa kwa upanga;umewaua bila huruma siku ya hasira yako.

22. Umewaalika kama kwenye sikukuumaadui zangu walionitisha kila upande.Katika siku ya hasira yako ee Mwenyezi-Mungu,hakuna aliyetoroka au kunusurika.Wale niliowazaa na kuwaleaadui zangu wamewaangamiza.

Kusoma sura kamili Maombolezo 2