Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 2:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Macho yangu yamevimba kwa kulia,roho yangu imechafuka.Moyo wangu una huzuni nyingikwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangukwa sababu watoto wachanga wanazirai katika barabara za mji.

12. Wanawalilia mama zao:“Wapi chakula, wapi kinywaji?”Huku wanazirai kama majeruhikatika barabara za mjini,na kukata roho mikononi mwa mama zao.

13. Nikuambie nini ee Yerusalemu?Nikulinganishe na nini?Nikufananishe na kitu ganiili niweze kukufariji,ee Siyoni uliye mzuri?Maafa yako ni mengi kama bahari.Ni nani awezaye kukuponya?

14. Manabii wako wamekuonea maono madanganyifu,hawakufichua wazi uovu wakoili wapate kukurekebisha,bali walikuonea kauli ya uongo na ya kupotosha.

15. Wapita njia wote wanakudhihaki;wanakuzomea, ee Yerusalemu,wakitikisa vichwa vyao kwa dharau na kusema:“Je, huu ndio ule mji uliofikia upeo wa uzuri,mji uliokuwa furaha ya dunia nzima?”

16. Maadui zako wote wanakuzomea,wanakufyonya na kukusagia meno,huku wakisema, “Tumemwangamiza!Kweli, siku ile tuliyoingojea kwa hamusasa imefika na tumeiona!”

17. Mwenyezi-Mungu amefanya yale aliyokusudia,ametekeleza yale aliyotishia;kama alivyopanga tangu kaleameangamiza bila huruma yoyote;amewafanya maadui wafurahie adhabu yako,amewakuza mashujaa wa maadui zako.

18. Kuta zako, ee mji wa Siyoni, zimlilie Mwenyezi-Mungu!Machozi na yatiririke kama mto mchana na usiku!Lia na kuomboleza bila kupumzika!

Kusoma sura kamili Maombolezo 2