Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 2:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yake,amewaweka watu wa Siyoni gizani.Fahari ya Israeli ameibwaga chini.Siku ya hasira yakealilitupilia mbali hata hekalu lake.

2. Mwenyezi-Mungu ameharibu bila hurumamakazi yote ya wazawa wa Yakobo.Kwa ghadhabu yake amezibomoa ngome za watu wa Yuda.Ufalme wao na watawala wakeameuporomosha chini kwa aibu.

3. Nguvu yote ya Israeli ameivunja kwa hasira.Hakunyosha mkono kuwasaidiawalipokutana na adui;amewawakia watu wa Yakobo kama moto,akateketeza kila kitu.

4. Amevuta upinde wake kama adui,na kuuweka mkono wake wa kulia tayari,amewaua wote tuliowaonea faharikatika maskani yetu watu wa Siyoni.Ametumiminia hasira yake kama moto.

5. Mwenyezi-Mungu amekuwa kama adui,ameangamiza watu wa Israeli;majumba yake yote ameyaharibu,ngome zake amezibomoa.Amewazidishia watu wa Yudamatanga na maombolezo.

6. Hekalu lake amelibomoa kama kitalu bustanini,maskani yake ameiharibu.Amefutilia mbali sikukuu na Sabato huko Siyoni,kwa hasira yake kuu amewakataa mfalme na makuhani.

7. Mwenyezi-Mungu ameipuuza madhabahu yakena hekalu lake amelikataa.Kuta za majumba mjini amewaachia maadui wazibomoe,wakapiga kelele humo nyumbani kwa Mwenyezi-Mungukama kelele za wakati wa sikukuu.

8. Mwenyezi-Mungu alipania kuubomoa ukuta wa mji wa Siyoni;aliupima na kuhakikisha kila kitu kimeharibiwa;minara na kuta za nje ya mji akazifanya ukiwa,zote kwa pamoja zikaangamia.

9. Malango yake yameanguka chini,makomeo yake ameyaharibu na kuyavunjavunja.Mfalme na wakuu wake wako uhamishoni kati ya mataifa.Mwongozo wa sheria umetoweka kabisa,manabii wake hawapati tena maonokutoka kwake Mwenyezi-Mungu.

10. Wazee wa Siyoni wameketi chini kimya,wamejitia mavumbi vichwanina kuvaa mavazi ya gunia.Wasichana wa Yerusalemu wameinamisha vichwa.

11. Macho yangu yamevimba kwa kulia,roho yangu imechafuka.Moyo wangu una huzuni nyingikwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangukwa sababu watoto wachanga wanazirai katika barabara za mji.

Kusoma sura kamili Maombolezo 2