Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 1:9-22 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Uchafu wake ulionekana waziwazi,lakini wenyewe haukujali mwisho wake.Anguko lake lilikuwa kubwa mno;hakuna awezaye kuufariji.Wasema:“Tazama ee Mwenyezi-Mungu mateso yangu,maana adui yangu ameshinda.”

10. Maadui wamenyosha mikono yao,wanyakue vitu vyake vyote vya thamani.Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni,watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakatazakujumuika na jumuiya ya watu wake.

11. Watu wa Yerusalemu wote wanahangaika kutafuta chakula;hazina zao wanazitoa kupata chakula,wajirudishie nguvu zao.Nao mji unalia,“Hebu niangalie, ee Mwenyezi-Mungu,ona jinsi nilivyogeuka kuwa duni.

12. “Enyi wapita njia, hivi hamjali kitu?Tazameni! Hakuna aliyepatwa na uchungu kama mimi,uchungu alioniletea Mwenyezi-Mungu,siku ya hasira yake kali.

13. “Aliteremsha moto kutoka juu,ukanichoma hata mifupani mwangu.Alinitegea wavu akaninasa,kisha akanirudisha nyuma,akaniacha nimeduwaa na kuzirai mchana kutwa.

14. “Aliyahesabu makosa yangu yoteakayakusanya mahali pamoja;aliyafunga shingoni mwangu kama nira,nikafyonzwa nguvu zangu kwa uzito wake.Mwenyezi-Mungu aliniweka mikononi mwaowatu ambao siwezi kuwapinga.

15. “Mwenyezi-Mungu aliwakataa askari walionilinda,alitangaza wakati maalumu wa kuniadhibukuwaponda vijana wangu wa kiume.Aliwaponda kama katika shinikizowatu wangu wa Yuda.

16. “Kwa sababu ya hayo ninalia,machozi yanitiririka,sina mtu yeyote wa kunifariji;hakuna yeyote wa kunitia moyo.Watoto wangu wameachwa wakiwa,maana adui yangu amenishinda.

17. “Nainyosha mikono yangulakini hakuna wa kunifariji.Mwenyezi-Mungu ametoa amri dhidi yangu mimi Yakobo,jirani zangu wawe maadui zangu.Naam, mimi Yerusalemu nimekuwa kinyaa kwao.

18. “Lakini Mwenyezi-Mungu amefanya sawakwa maana nimeliasi neno lake.Nisikilizeni enyi watu wote,yatazameni mateso yangu.Wasichana wangu na wavulana wangu,wamechukuliwa mateka.

19. “Niliwaita wapenzi wangu,lakini wao wakanihadaa.Makuhani na wazee wanguwamefia mjiniwakijitafutia chakula,ili wajirudishie nguvu zao.

20. “Ona, ee Mwenyezi-Mungu nilivyo taabuni.Roho yangu imechafuka,moyo wangu unasononekakwani nimekuasi vibaya.Huko nje kumejaa mauaji,ndani nako ni kama kifo tu.

21. “Sikiliza ninavyopiga kite;hakuna wa kunifariji.Maadui zangu wote wamesikia juu ya taabu yangu:Wanafurahi kwamba umeniletea maafa.Uifanye ile siku uliyoahidi ifike,uwafanye nao wateseke kama mimi.

22. “Uwapatilize kwa ajili ya uovu wao wote.Uwatende kama ulivyonitenda mimikwa sababu ya makosa yangu yote.Nasononeka sana kwa maumivuna moyo wangu unazimia.”

Kusoma sura kamili Maombolezo 1