Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 1:7-19 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Ukiwa sasa magofu matupu,Yerusalemu wakumbuka fahari yake.Ulipoangukia mikononi mwa maadui zake,hakuna aliyekuwako kuusaidia.Washindi wake walichekelea kuanguka kwake.

8. Yerusalemu ulitenda dhambi mbaya,ukawa mchafu kwa dhambi zake.Wote waliousifia wanaudharau,maana wameuona uchi wake.Wenyewe wapiga kite na kujificha kwa aibu.

9. Uchafu wake ulionekana waziwazi,lakini wenyewe haukujali mwisho wake.Anguko lake lilikuwa kubwa mno;hakuna awezaye kuufariji.Wasema:“Tazama ee Mwenyezi-Mungu mateso yangu,maana adui yangu ameshinda.”

10. Maadui wamenyosha mikono yao,wanyakue vitu vyake vyote vya thamani.Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni,watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakatazakujumuika na jumuiya ya watu wake.

11. Watu wa Yerusalemu wote wanahangaika kutafuta chakula;hazina zao wanazitoa kupata chakula,wajirudishie nguvu zao.Nao mji unalia,“Hebu niangalie, ee Mwenyezi-Mungu,ona jinsi nilivyogeuka kuwa duni.

12. “Enyi wapita njia, hivi hamjali kitu?Tazameni! Hakuna aliyepatwa na uchungu kama mimi,uchungu alioniletea Mwenyezi-Mungu,siku ya hasira yake kali.

13. “Aliteremsha moto kutoka juu,ukanichoma hata mifupani mwangu.Alinitegea wavu akaninasa,kisha akanirudisha nyuma,akaniacha nimeduwaa na kuzirai mchana kutwa.

14. “Aliyahesabu makosa yangu yoteakayakusanya mahali pamoja;aliyafunga shingoni mwangu kama nira,nikafyonzwa nguvu zangu kwa uzito wake.Mwenyezi-Mungu aliniweka mikononi mwaowatu ambao siwezi kuwapinga.

15. “Mwenyezi-Mungu aliwakataa askari walionilinda,alitangaza wakati maalumu wa kuniadhibukuwaponda vijana wangu wa kiume.Aliwaponda kama katika shinikizowatu wangu wa Yuda.

16. “Kwa sababu ya hayo ninalia,machozi yanitiririka,sina mtu yeyote wa kunifariji;hakuna yeyote wa kunitia moyo.Watoto wangu wameachwa wakiwa,maana adui yangu amenishinda.

17. “Nainyosha mikono yangulakini hakuna wa kunifariji.Mwenyezi-Mungu ametoa amri dhidi yangu mimi Yakobo,jirani zangu wawe maadui zangu.Naam, mimi Yerusalemu nimekuwa kinyaa kwao.

18. “Lakini Mwenyezi-Mungu amefanya sawakwa maana nimeliasi neno lake.Nisikilizeni enyi watu wote,yatazameni mateso yangu.Wasichana wangu na wavulana wangu,wamechukuliwa mateka.

19. “Niliwaita wapenzi wangu,lakini wao wakanihadaa.Makuhani na wazee wanguwamefia mjiniwakijitafutia chakula,ili wajirudishie nguvu zao.

Kusoma sura kamili Maombolezo 1