Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 1:10-16 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Maadui wamenyosha mikono yao,wanyakue vitu vyake vyote vya thamani.Naam umeona watu wa mataifa wakiingia hekaluni,watu ambao Mwenyezi-Mungu aliwakatazakujumuika na jumuiya ya watu wake.

11. Watu wa Yerusalemu wote wanahangaika kutafuta chakula;hazina zao wanazitoa kupata chakula,wajirudishie nguvu zao.Nao mji unalia,“Hebu niangalie, ee Mwenyezi-Mungu,ona jinsi nilivyogeuka kuwa duni.

12. “Enyi wapita njia, hivi hamjali kitu?Tazameni! Hakuna aliyepatwa na uchungu kama mimi,uchungu alioniletea Mwenyezi-Mungu,siku ya hasira yake kali.

13. “Aliteremsha moto kutoka juu,ukanichoma hata mifupani mwangu.Alinitegea wavu akaninasa,kisha akanirudisha nyuma,akaniacha nimeduwaa na kuzirai mchana kutwa.

14. “Aliyahesabu makosa yangu yoteakayakusanya mahali pamoja;aliyafunga shingoni mwangu kama nira,nikafyonzwa nguvu zangu kwa uzito wake.Mwenyezi-Mungu aliniweka mikononi mwaowatu ambao siwezi kuwapinga.

15. “Mwenyezi-Mungu aliwakataa askari walionilinda,alitangaza wakati maalumu wa kuniadhibukuwaponda vijana wangu wa kiume.Aliwaponda kama katika shinikizowatu wangu wa Yuda.

16. “Kwa sababu ya hayo ninalia,machozi yanitiririka,sina mtu yeyote wa kunifariji;hakuna yeyote wa kunitia moyo.Watoto wangu wameachwa wakiwa,maana adui yangu amenishinda.

Kusoma sura kamili Maombolezo 1