Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 1:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ajabu mji uliokuwa umejaa watu,sasa wenyewe umebaki tupu!Ulikuwa maarufu kati ya mataifa;sasa umekuwa kama mama mjane.Miongoni mwa miji ulikuwa kama binti mfalme;sasa umekuwa mtumwa wa wengine.

2. Walia usiku kucha;machozi yautiririka.Hakuna hata mmoja wa wapenzi wake wa kuufariji.Rafiki zake wote wameuhadaa;wote wamekuwa adui zake.

3. Watu wa Yuda wamekwenda uhamishonipamoja na mateso na utumwa mkali.Sasa wanakaa miongoni mwa watu wa mataifa,wala hawapati mahali pa kupumzika.Waliowafuatia wamewakamata wakiwa taabuni.

4. Barabara za kwenda Siyoni zinasikitisha;hakuna wapitao kwenda kwenye sikukuu.Malango ya mji wa Siyoni ni tupu;makuhani wake wanapiga kite,wasichana wake wana huzuni,na mji wenyewe uko taabuni.

5. Adui zake ndio wanaoutawala na wanafanikiwa,kwani Mwenyezi-Mungu ameutesakwa sababu ya makosa mengi.Watoto wake wametekwa na kupelekwa mbali.

6. Fahari yote ya watu wa Siyoni imewatoweka;wakuu wake wamekuwa kama kulungu wasio na malisho.Bila nguvu waliwakimbia watesi wao.

7. Ukiwa sasa magofu matupu,Yerusalemu wakumbuka fahari yake.Ulipoangukia mikononi mwa maadui zake,hakuna aliyekuwako kuusaidia.Washindi wake walichekelea kuanguka kwake.

Kusoma sura kamili Maombolezo 1