Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 38:14-18 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Chandarua cha kila upande wa mlango kilikuwa na upana wa mita 6.5, pamoja na nguzo tatu na vikalio vyake vitatu.

15. Upande mwingine kadhalika ulikuwa na chandarua chenye upana wa mita 6.5, pamoja na nguzo tatu na vikalio vyake vitatu.

16. Vyandarua vyote kuuzunguka ua vilikuwa vya kitani safi iliyosokotwa.

17. Vikalio vyote vya nguzo vilikuwa vya shaba, lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha. Matumba yake yalikuwa ya fedha; pia nguzo zake zote zilishikamanishwa kwa fito za fedha.

18. Pazia la mlango wa ua lilitengenezwa kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi iliyosokotwa, na kutariziwa vizuri; nalo lilikuwa na urefu wa mita 9 na kimo cha mita 2, kulingana na vyandarua vya ua.

Kusoma sura kamili Kutoka 38