Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 33:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hii ndiyo baraka ambayo Mose, mtu wa Mungu aliwatakia Waisraeli kabla ya kufariki kwake. Alisema:

2. Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai,alitutokea kutoka mlima Seiri;aliiangaza kutoka mlima Parani.Alitokea kati ya maelfu ya malaika,na moto uwakao katika mkono wake wa kulia.

3. Mwenyezi-Mungu aliwapenda watu wake;na huwalinda watakatifu wake wote.Hivyo, malaika wake walifuata nyayo zake,na kupata maagizo kutoka kwake.

4. Mose alituamuru tutii sheria;kitu cha thamani kuu cha taifa letu.

5. Mwenyezi-Mungu akawa mfalme wa Israeli,wakati viongozi wao walipokutana,na makabila yote yalipokusanyika.

6. Mose alisema juu ya kabila la Reubeni:“Reubeni aishi wala asife,na watu wake wasiwe wachache.”

7. Juu ya kabila la Yuda alisema:“Ee Mwenyezi-Mungu usikilize kilio cha kabila la Yuda;umrudishe tena kwa watu wale wengine.Upigane kwa mikono yako kwa ajili yake,ulisaidie kabila la Yuda dhidi ya adui zake.”

8. Juu ya kabila la Lawi, alisema:“Ee Mwenyezi-Mungu ulipatie Lawi kauli yako ya Urimu,kauli yako ya thumimu kwa hao waaminifu wako,ambao uliwajaribu huko Masa.

9. Ulishindana nao kwenye maji ya Meriba.Walawi walioamua kuwaacha wazee wao,wakawasahau jamaa zao,wasiwatambue hata watoto waomaana walizingatia amri zako,na kushika agano lako.

10. Na wawafundishe wazawa wa Yakobo maagizo yako;wawafundishe watu wa Israeli sheria yako.Walawi na wafukize ubani mbele yako,sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni pako.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 33