Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 32:8-24 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao,alipowagawa wanadamu,kila taifa alilipatia mipaka yake,

9. kulingana na idadi ya watoto wa Mungu,lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake,hao alijichagulia kuwa mali yake.

10. Aliwakuta katika nchi ya jangwa,nyika tupu zenye upepo mkali.Aliwalinda na kuwatunza,aliwafanya kama mboni ya jicho lake.

11. Kama tai alindaye kiota chake,na kurukaruka juu ya makinda yake,akitandaza mabawa yake ili kuwashikilia,na kuwabeba juu ya mabawa yake.

12. Yeye Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwaongozana hapakuwa na mungu mwingine wa kumsaidia.

13. Aliwapitisha katika nyanda za juu za nchi,nao wakala mazao ya mashambani.Akawapa asali miambani waonjena mafuta kutoka mwamba mgumu.

14. Aliwapa siagi na maziwa ya mifugo,mafuta ya wanakondoo na kondoo madume,makundi ya mifugo ya Bashani na mbuzi.Aliwapa ngano nzuri kabisa na divai mpya wakanywa.

15. Watu wa Israeli walinona na kupiga mateke;walinenepa, wakawa na kitambi na kunawiri;kisha wakamwacha Mungu aliyewaumba,wakamdharau Mwamba wa wokovu wao.

16. Walimfanya aone wivu mkali kwa miungu yao,walimchochea akasirike kwa matendo yao ya kuchukiza.

17. Walitambikia majini ambayo hayakuwa miungu,waliiendea miungu ambayo hawakuijua kamwe,miungu mipya iliyotokea siku za karibuni,ambayo wazee wao hawakuiheshimu kamwe.

18. Hamkumjali Mwamba aliyewapa uhai,mlimsahau Mungu aliyewazaa nyinyi.

19. Mwenyezi-Mungu aliona jambo hilo akawaacha;aliwakataa watoto wake, waume kwa wake.

20. Akasema, ‘Nitawaficha uso wangunione mwisho wao utakuwaje!Maana wao ni kizazi kipotovu,watoto wasio na uaminifu wowote.

21. Wamenichochea kuona wivu kwa kitu kisicho mungu,wamenikasirisha kwa sanamu zao.Hivyo nitawafanya waone wivu kwa kisicho watu,nitawakasirisha kwa kutumia taifa la wapumbavu.

22. Hasira yangu imewaka moto,inachoma mpaka chini kuzimu,itateketeza dunia na vilivyomo,itaunguza misingi ya milima.

23. Nitarundika maafa chungu nzima juu yao,nitawamalizia mishale yangu.

24. Watakonda kwa njaa,wataangamizwa kwa homa kali.Nitapeleka wanyama wenye meno makali kuwashambulia,na nyoka wenye sumu wanaotambaa mavumbini.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 32