Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 25:10-19 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Na jina la nyumba yake katika Israeli litakuwa: ‘Nyumba ya mtu aliyevuliwa kiatu.’”

11. “Wanaume wawili wakipigana na mke wa mmoja wao akamsaidia mumewe kwa kumkamata sehemu za siri yule anayepigana na mumewe,

12. mtaukata mkono wa kulia wa huyo mwanamke; msimhurumie.

13. “Msiwe na vipimo vya kupimia vya namna mbili: Kimoja kizito na kingine chepesi. Msitumie mizani za udanganyifu.

14. Wala msiwe na aina mbili za vipimo vya kupimia, kubwa na ndogo.

15. “Tumieni mizani na vipimo vyenye uzito sahihi ili mpate kuishi maisha marefu katika nchi anayowapa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.

16. Wote wanaofanya mambo hayo, wote wanaotenda kwa udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.

17. “Kumbukeni kitendo cha Waamaleki mlipokuwa safarini kutoka Misri.

18. Kumbukeni walivyowashambulieni huko njiani mkiwa wanyonge na kuwapiga wale wote waliokuja nyuma yenu wamechoka. Waamaleki hawakumwogopa Mungu.

19. Kwa hiyo wakati Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapowapumzisha kutokana na mashambulio ya adui zenu wote wanaowazunguka katika nchi ambayo amewapa mwimiliki na kuishi humo, ni lazima muwaangamize Waamaleki wote.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 25