Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 25:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Ikiwa kuna ugomvi kati ya watu wawili, wakaenda kuamuliwa mahakamani, mmoja akaonekana hana hatia, na mwingine akahukumiwa,

2. kama yule aliyehukumiwa amepewa adhabu ya kuchapwa viboko, hakimu atamwamuru huyo alale chini na kuchapwa viboko kulingana na kosa lake.

3. Mwenye hatia anaweza kuchapwa viboko arubaini lakini si zaidi. Mkizidisha kiasi hicho mtakuwa mmemfedhehesha ndugu yenu.

4. “Usimfunge ng'ombe kinywa anapopura nafaka.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 25