Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 9:7-21 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Utawala wake utastawi daima,amani ya ufalme wake haitakoma.Atachukua wadhifa wa mfalme Daudina kutawala juu ya ufalme wake;ataustawisha na kuuimarisha,kwa haki na uadilifu,tangu sasa na hata milele.Hayo atayafanya Mwenyezi-Mungu wa majeshi.

8. Mwenyezi-Mungu ametoa tamko dhidi ya Yakobonalo litampata Israeli.

9. Watu wote watatambua,ukoo wote wa Efraimuna wakazi wa Samaria.Kwa kiburi na majivuno wanasema:

10. “Kuta za matofali zimeangukalakini sisi tutazijenga kwa mawe yaliyochongwa!Nyumba za boriti za mikuyu zimeharibiwalakini mahali pake tutajenga za mierezi.”

11. Basi, Mwenyezi-Mungu atawaletea wapinzanina kuwachochea maadui zao.

12. Waaramu upande wa mashariki,Wafilisti upande wa magharibi,wamepanua vinywa vyao kuimeza Israeli.Hata hivyo, hasira yake haijatulia,bado ameunyosha mkono wake.

13. Ingawa aliwaadhibu watu,hawakumrudia Mwenyezi-Mungu wa majeshi.

14. Basi kwa muda wa siku moja tu,Mwenyezi-Mungu atakata katika Israeli vichwa na mikia,tawi la mtende na nyasi:

15. Vichwa ndio wazee na waheshimiwa,mikia ndio manabii wafundishao uongo.

16. Wale wanaoongoza watu hawa wamewapotosha,na hao wanaoongozwa nao wamepotoka.

17. Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu hawahurumii vijana wao,hana huruma juu ya yatima na wajane wao;kwani hakuna hata mmoja amchaye Mungu,kila mtu husema uongo.Hata hivyo, hasira yake haijatulia,bado ameunyosha mkono wake.

18. Uovu huwaka kama motouteketezao mbigili na miiba;huwaka kama moto msituni,na kutoa moshi mzito upandao angani juu.

19. Kwa ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu wa majeshinchi imechomwa moto,na watu ni kama kuni za kuuwasha.Hakuna mtu anayemhurumia ndugu yake;

20. wananyanganya upande mmoja na hawatosheki;wanakula upande mwingine lakini hawashibi.Kila mmoja anamshambulia mwenzake.

21. Manase dhidi ya Efraimu,Efraimu dhidi ya Manasena wote wawili dhidi ya Yuda.Hata hivyo, hasira ya Mwenyezi-Mungu haijatulia,bado ameunyosha mkono wake.

Kusoma sura kamili Isaya 9