Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 9:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Lakini nchi ile iliyokuwa imekumbwa na huzuni haitabaki daima katika giza hilo kuu. Hapo awali Mungu alizifedhehesha nchi za Zebuluni na Naftali, lakini siku za usoni ataifanikisha sehemu hii ya baharini na nchi iliyo ngambo ya Yordani na hata Galilaya wanamoishi watu wa mataifa.

2. Watu waliotembea gizaniwameona mwanga mkubwa.Watu walioishi katika nchi ya giza kuu,sasa mwanga umewaangazia.

3. Wewe, ee Mungu, umelikuza taifa,umeiongeza furaha yake.Watu wanafurahi mbele yako,wana furaha kama wakati wa mavuno,kama wafurahivyo wanaogawana nyara.

Kusoma sura kamili Isaya 9