Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 66:9-13 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe,halafu niwazuie wasizaliwe?Au mimi mwenye kuwajalia watoto,nitafunga kizazi chao?Mimi Mungu wenu nimesema.”

10. Shangilieni na kufurahi pamoja na Yerusalemu enyi mnaoupenda!Shangilieni pamoja nao enyi nyote mlioulilia!

11. Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha,nanyi mtashiba kwa riziki zake;mtakunywa shibe yenu na kufurahi,kutokana na wingi wa fahari yake.

12. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitakuletea fanaka nyingi kama mto,utajiri wa mataifa kama mto uliofurika.Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga,mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake.

13. Kama mama amtulizavyo mwanawe,kadhalika nami nitawatuliza;mtatulizwa mjini Yerusalemu.

Kusoma sura kamili Isaya 66