Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 66:7-14 Biblia Habari Njema (BHN)

7. “Mji wangu mtakatifu,ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu;kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto.

8. Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo?Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo?Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja?Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja?Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu,alijifungua watoto wake.

9. Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe,halafu niwazuie wasizaliwe?Au mimi mwenye kuwajalia watoto,nitafunga kizazi chao?Mimi Mungu wenu nimesema.”

10. Shangilieni na kufurahi pamoja na Yerusalemu enyi mnaoupenda!Shangilieni pamoja nao enyi nyote mlioulilia!

11. Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha,nanyi mtashiba kwa riziki zake;mtakunywa shibe yenu na kufurahi,kutokana na wingi wa fahari yake.

12. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitakuletea fanaka nyingi kama mto,utajiri wa mataifa kama mto uliofurika.Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga,mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake.

13. Kama mama amtulizavyo mwanawe,kadhalika nami nitawatuliza;mtatulizwa mjini Yerusalemu.

14. Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi;mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi.Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu,lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”

Kusoma sura kamili Isaya 66