Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 66:19-24 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Nitaweka kati yao alama ya uwezo wangu. Watakaosalimika kati yao nitawapeleka kwa watu wa mataifa huko Tarshishi, Puti, Ludi, nchi zenye wapiga upinde stadi; watakwenda pia Tubali na Yowani na nchi ambapo watu hawajapata kusikia umaarufu wangu wala kuuona utukufu wangu. Hao wajumbe wangu watautangaza utukufu wangu katika mataifa hayo.

20. Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.

21. Pia nitawachagua baadhi yao kuwa makuhani na baadhi yao kuwa Walawi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

22. “Kama vile mbingu mpya na dunia mpya nitakazoumbazitakavyodumu milele kwa uwezo wangu,ndivyo wazawa wako na jina lako litakavyodumu.

23. Katika kila sikukuu ya mwezi mpya,na katika kila siku ya Sabato,binadamu wote watakuja kuniabudu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

24. “Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”

Kusoma sura kamili Isaya 66