Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 66:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Kama mama, Yerusalemu utawanyonyesha,nanyi mtashiba kwa riziki zake;mtakunywa shibe yenu na kufurahi,kutokana na wingi wa fahari yake.

12. Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitakuletea fanaka nyingi kama mto,utajiri wa mataifa kama mto uliofurika.Nanyi mtanyonya na kubebwa kama mtoto mchanga,mtabembelezwa kama mtoto magotini mwa mama yake.

13. Kama mama amtulizavyo mwanawe,kadhalika nami nitawatuliza;mtatulizwa mjini Yerusalemu.

14. Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi;mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi.Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu,lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”

15. Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto,na magari yake ya vita ni kimbunga.Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali,na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto.

16. Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto,atawaadhibu watu wote kwa upanga;nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.

17. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wapo watu wanaojitakasa na kutawadha wapate kuingia kwenye bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kuhani akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu. Watu hao hakika watakufa wote pamoja.

Kusoma sura kamili Isaya 66