Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 65:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yaowayalipie na maovu ya wazee wao.Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani,wakanitukana mimi huko vilimani.Nitawafanya walipe kwa wingi,watayalipia matendo yao ya awali.”

8. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri,watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;sitawaangamiza wote.

9. Nitawajalia watu wa Yakobo,na Yuda nitamjalia warithi wa milima yangu;watumishi wangu watakaa huko.

10. Nchi tambarare ya Sharoni itakuwa malisho,bonde la Akori litakuwa mapumziko ya mifugokwa ajili ya watu wangu walionitafuta.

11. “Lakini nitafanya nini na nyinyimnaoniacha mimi Mwenyezi-Mungu,msioujali Siyoni, mlima wangu mtakatifu,nyinyi mnaoabudu mungu ‘Gadi’,na kumtolea tambiko ya divai mungu ‘Meni’?

12. Nimewapangia kifo kwa upanga,nyote mtaangukia machinjoni!Maana, nilipowaita, hamkuniitikia;niliponena, hamkunisikiliza.Mlitenda yaliyo maovu mbele yangu,mkachagua yale nisiyoyapenda.

Kusoma sura kamili Isaya 65