Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 65:18-25 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Furahini, mkashangilie milele,kwa ajili ya vitu hivi ninavyoumba.Yerusalemu nitaufanya mji wa shangwe,na watu wake watu wenye furaha.

19. Nami nitaufurahia mji wa Yerusalemu,nitawafurahia watu wangu.Sauti ya kilio haitasikika tena,kilio cha taabu hakitakuwako.

20. Hakutakuwa tena na vifo vya watoto wachanga,wazee nao hawatakufa kabla ya wakati wao.Akifa mtu wa miaka 100 amekufa akiwa kijana;na akifa kabla ya miaka 100 ni balaa.

21. Watu watajenga nyumba na kuishi humo;watalima mizabibu na kula matunda yake.

22. Hawatajenga nyumba zikaliwe na watu wengine,wala kulima chakula kiliwe na watu wengine.Maana watu wangu niliowachaguawataishi maisha marefu kama miti;wateule wangu watafurahia matunda ya jasho lao.

23. Kazi zao hazitakuwa bure,wala hawatazaa watoto wa kupata maafa;maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu,wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.

24. Hata kabla hawajaniita, mimi nitawaitikia;kabla hawajamaliza kusema, nitakuwa nimewajibu.

25. Mbwamwitu na kondoo watakula pamoja,simba watakula nyasi kama ng'ombe,nao nyoka chakula chao kitakuwa vumbi.Katika mlima wangu wote mtakatifu,hakuna atakayeumiza au kuharibu kitu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Kusoma sura kamili Isaya 65