Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 65:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema;“Nilikuwa tayari kujioneshakwao wasiouliza habari zangu.Nilikuwa tayari kuwapokeawale wasionitafuta.Nililiambia taifa ambalo halikuomba kwa jina langu:‘Nipo hapa! Nipo hapa!’

2. Mchana kutwa niliwanyoshea mikono watu waasi,watu ambao hufuata njia zisizo sawa,watu ambao hufuata fikira zao wenyewe.

3. Ni watu ambao daima hunichokoza waziwazi;hutambikia miungu yao katika bustani,na kuifukizia ubani juu ya matofali.

4. Huketi makaburini na kukaa mafichoni usiku.Hula nyama ya nguruwe na mchuzi wa wanyama haramu.

5. Huwaambia wale wanaokutana nao:‘Kaeni mbali nami;msinikaribie kwani mimi ni mtakatifu!’Watu hao wananikasirisha mno,hasira yangu ni kama moto usiozimika.

6. “Jueni kuwa nimelitia jambo hilo moyoni,sitanyamaza bali nitawafanya walipe;nitawafanya walipe kwa wingi.

7. Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yaowayalipie na maovu ya wazee wao.Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani,wakanitukana mimi huko vilimani.Nitawafanya walipe kwa wingi,watayalipia matendo yao ya awali.”

8. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri,watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;sitawaangamiza wote.

9. Nitawajalia watu wa Yakobo,na Yuda nitamjalia warithi wa milima yangu;watumishi wangu watakaa huko.

10. Nchi tambarare ya Sharoni itakuwa malisho,bonde la Akori litakuwa mapumziko ya mifugokwa ajili ya watu wangu walionitafuta.

Kusoma sura kamili Isaya 65