Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 55:9-13 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Kama vile mbingu zilivyo mbali na dunia,ndivyo njia zangu zilivyo mbali na zenu,na mawazo yangu mbali na mawazo yenu.

10. “Kama vile mvua na theluji ishukavyo toka mbinguni,wala hairudi huko bali huinywesha ardhi,ikaifanya ichipue mimea ikakua,ikampatia mpanzi mbegu na kuwapa watu chakula,

11. vivyo hivyo na neno langu mimi:Halitanirudia bila mafanikio,bali litatekeleza matakwa yangu,litafanikiwa lengo nililoliwekea.

12. “Mtatoka Babuloni kwa furaha;mtaongozwa mwende kwa amani.Milima na vilima mbele yenu vitapaza sauti na kuimba,na miti yote mashambani itawapigia makofi.

13. Badala ya michongoma kutamea misonobari,na badala ya mbigili kutamea mihadasi.Hilo litakuwa jambo litakalowakumbusha watujuu ya mambo niliyotenda mimi Mwenyezi-Mungu;ishara ya milele ambayo haitafutwa.”

Kusoma sura kamili Isaya 55