Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 55:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. “Tegeni sikio enyi watu wangu, mje kwangu;nisikilizeni, ili mpate kuishi.Nami nitafanya nanyi agano la milele;nitawapeni fadhili nilizomwahidi Daudi.

4. Mimi nilimfanya kiongozi na kamanda wa mataifaili yeye anishuhudie kwa watu wa mataifa.

5. Sasa utayaita mataifa usiyoyajua,watu wa mataifa yasiyokutambua watakujia mbio,kwa sababu yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;kwa sababu yangu mimi Mtakatifu wa Israeliniliyekufanya wewe utukuke.”

6. Mtafuteni Mwenyezi-Mungu wakati bado anapatikana,mwombeni msaada wakati yupo bado karibu.

Kusoma sura kamili Isaya 55