Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 50:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Mgongo wangu niliwaachia walionipiga,mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu;walioniaibisha na kunitemea mate,sikujificha mbali nao.

7. Bwana Mungu hunisaidia,kwa hiyo siwezi kufadhaika.Uso wangu nimeukaza kama jiwe;najua kwamba sitaaibishwa.

8. Mtetezi wangu yuko karibu.Ni nani atakayepingana nami?Na aje tusimame mahakamani.Adui yangu ni nani?Na ajitokeze mbele basi.

9. Tazama Bwana Mungu hunisaidia.Ni nani awezaye kusema nina hatia?Maadui zangu wote watachakaa kama vazi,nondo watawatafuna.

Kusoma sura kamili Isaya 50