Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 49:13-20 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Imbeni kwa furaha, enyi mbingu!Shangilia ewe dunia.Pazeni sauti mwimbe enyi milima,maana Mwenyezi-Mungu amewafariji watu wake,naam, atawaonea huruma watu wake wanaoteseka.

14. Wewe Siyoni wasema:“Mwenyezi-Mungu ameniacha;hakika Bwana wangu amenisahau.”

15. Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Je, mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya,asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake?Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe,mimi kamwe sitakusahau.

16. Nimekuchora katika viganja vyangu;kuta zako naziona daima mbele yangu.

17. Watakaokujenga upya wanakuja haraka,wale waliokuharibu wanaondoka.

18. Inua macho uangalie pande zote;watu wako wote wanakusanyika na kukujia.Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu,watu wako watakuwa kwako kama mapambo,utawafurahia kama afanyavyo bibi arusi na utaji wake.

19. “Kweli umekumbana na uharibifu,makao yako yamekuwa matupu,na nchi yako imeteketezwa.Lakini sasa itakuwa ndogo mno kwa wakazi wake;na wale waliokumaliza watakuwa mbali.

20. Wanao waliozaliwa uhamishoni,watakulalamikia wakisema:‘Nchi hii ni ndogo mno;tupatie nafasi zaidi ya kuishi.’

Kusoma sura kamili Isaya 49