Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 49:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nisikilizeni, enyi nchi za mbali,tegeni sikio, enyi watu wa mbali!Mwenyezi-Mungu aliniita kabla sijazaliwa,alitaja jina langu nikiwa tumboni mwa mama yangu.

2. Aliyapa ukali maneno yangu kama upanga mkali,alinificha katika kivuli cha mkono wake;aliufanya ujumbe wangu mkali kama ncha ya mshale,akanificha katika podo lake.

3. Aliniambia, “Wewe ni mtumishi wangu;kwako, Israeli, watu watanitukuza.”

4. Lakini mimi nikafikiri,“Nimeshughulika bure,nimetumia nguvu zangu bure kabisa.”Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu atanipa haki yangu;tuzo la kazi yangu liko kwa Mungu.

5. Lakini asema sasa Mwenyezi-Mungu,ambaye aliniita tangu tumboni mwa mama yanguili nipate kuwa mtumishi wake;nilirudishe taifa la Yakobo kwake,niwakusanye wazawa wa Israeli kwake.Mwenyezi-Mungu amenijalia heshima mbele yake.Mungu wangu amekuwa ndiye nguvu yangu.

6. Yeye asema: “Haitoshi tu wewe kuwa mtumishi wangu,uyainue makabila ya Yakobo,na kurekebisha watu wa Israeli waliobaki.Nitakufanya uwe mwanga wa mataifa,niwaletee wokovu watu wote duniani.”

7. Mwenyezi-Mungu, Mkombozi na Mtakatifu wa Israeli,amwambia hivi yule anayedharauliwa mno,yule anayechukiwa na mataifa,na ambaye ni mtumishi wa watawala:“Wafalme watakuona nao watasimama kwa heshima,naam, wakuu watainama na kukusujudiakwa sababu yangu mimi Mwenyezi-Munguambaye hutimiza ahadi zangu;kwa sababu yangu mimi Mtakatifu wa Israeliambaye nimekuteua wewe.”

8. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wakati wa kufaa nilikujibu ombi lako;wakati wa wokovu nilikusaidia.Nimekuweka na kukufanyauwe kiungo cha agano langu na mataifa yote:Kuirekebisha nchi iliyoharibika,na kuwarudishia wenyewe ardhi hiyo;

9. kuwaambia wafungwa, ‘Tokeni humo gerezani’,na wale walio gizani, ‘Njoni nje mwangani!’Kila mahali watakapokwenda watapata chakulahata kwenye vilima vitupu watapata malisho.

Kusoma sura kamili Isaya 49