Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 48:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Ninafanya hivyo kwa ajili yangu mwenyewe.Kwa nini jina langu lidharauliwe?Utukufu wangu siwezi kumpa mwingine!

12. “Nisikilize ee taifa la Yakobo,nisikilize ee Israeli niliyekuita.Mimi ndiye Mungu;mimi ni wa kwanza na wa mwisho.

13. Kwa mkono wangu niliuweka msingi wa dunia,mimi mwenyewe nilizitandaza mbingu.Nikiziita mbingu na dunia,zinasimama haraka mbele yangu.

14. “Kusanyikeni nyote msikilize!Nani kati ya miungu yenu aliyetabiri vitu hivi?Mimi Mwenyezi-Mungu nampenda Koreshi;yeye atatekeleza lengo langu kuhusu Babuloni,naam, yeye atawashambulia Wakaldayo.

15. Mimi, naam, mimi nimeyasema na kumwita;nimemleta, naye atafaulu katika mpango wake.

16. Njoni karibu nami msikie jambo hili:Tangu mwanzo mimi sikusema kwa siri,tangu mambo hayo yaanze kutendeka, nimekuwapo.”Sasa, Bwana Mungu amenituma,na kunipa nguvu ya roho yake.

17. Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli,Mkombozi wako, asema hivi:“Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,ninayekufundisha kwa faida yako,ninayekuongoza katika njia unayotakiwa kwenda.

18. Laiti ungalizitii amri zangu!Hapo baraka zingekutiririkia kama mto,ungepata fanaka kwa wingi kama mawimbi ya bahari.

Kusoma sura kamili Isaya 48