Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 48:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sikilizeni, enyi watu wa Yakobo,enyi mnaojulikana kwa jina la Israeli,nyinyi mlio wa ukoo wa Yuda.Nyinyi huapa kwa jina la Mwenyezi-Mungu,na kudai mnamwabudu Mungu wa Israeli;lakini hayo si ukweli wala sawa.

2. Nyinyi mnaona fahari kujiita watu wa mji mtakatifu,na kujidai kumtegemea Mungu wa Israeli,ambaye jina lake ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi.

3. “Nilitangaza zamani matukio ya awali,niliyatamka mimi mwenyewena kuyafanya yajulikane kwenu.Mara nikaanza kuyatekeleza,nayo yakapata kutukia.

4. Lakini nilikujua wewe kuwa mkaidi;kichwa kigumu kama chuma,uso wako mkavu kama shaba.

5. Kwa hiyo nilikutangazia tangu zamani,kabla hayajatukia mimi nilikutangazia,usije ukasema, ‘Kinyago changu kiliyatenda hayo,sanamu zangu za kuchonga na kusubu ziliyafanya.’

6. “Wewe uliyasikia na sasa unayaona yote.Kwa nini huwezi kuyakiri?Tangu sasa nitakujulisha mambo mapya;mambo yaliyofichika ambayo hukuyajua.

7. Mambo hayo yanatukia sasa;hukupata kuyasikia kabla ya leo,hivyo huwezi kusema, ‘Aa! Nilikwisha yajua.’

8. Hujapata kamwe kuyasikia wala kuyajua;tangu zamani masikio yako hayakuyasikia.Nilijua kuwa wewe ni mwenye hila,na kwamba wewe ni mwasi tangu kuzaliwa.

9. “Kwa heshima ya jina langu,ninaiahirisha hasira yangu;kwa ajili ya heshima yangu,ninaizuia nisije nikakuangamiza.

10. Mimi nitawajaribu lakini si kama fedha katika tanuri.Nitawajaribu katika tanuri ya taabu.

Kusoma sura kamili Isaya 48