Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 47:3-12 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Watu watauona uchi wako;naam, wataiona aibu yako.Mimi nitalipiza kisasi,wala sitamhurumia yeyote.”

4. Mkombozi wetu ndiye Mtakatifu wa Israeli;Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

5. Mwenyezi-Mungu asema:“Ewe taifa la Wakaldayolililo kama binti mzuri,keti kimya na kutokomea gizani.Maana umepoteza hadhi yakoya kuwa bimkubwa wa falme.

6. Niliwakasirikia watu wangu Israeli,nikawafanya watu wangu kuwa haramu.Niliwatia mikononi mwako,nawe hukuwaonea huruma;na wazee uliwatwisha nira nzito mno.

7. Ulijisemea moyoni: ‘Nitakuwa malkia milele’,nawe hukuyatafakari mambo yanayotokea,wala kufikiri mwisho wake.

8. “Sasa, basi, sikiliza ewe mpenda anasa,wewe unayedhani kuwa u salama,na kujisemea: ‘Ni mimi tu,na hakuna mwingine isipokuwa mimi.Kamwe sitakuwa mjane,wala sitafiwa na wanangu.’

9. Haya yote mawili yatakupata,ghafla, katika siku moja:Kupoteza watoto wako na kuwa mjane,ijapokuwa una wingi wa uchawi wako,na nguvu nyingi za uganga wako.

10. “Ulijiona salama katika uovu wako;ukajisemea, ‘Hakuna mtu anayeniona.’Hekima na elimu yako vilikupotosha,ukajisemea moyoni mwako, ‘Mimi ndiye;hakuna mwingine anayenishinda.’

11. Lakini maafa yatakupataambayo hutaweza kujiepusha nayo.Balaa litakukumbaambalo hutaweza kulipinga;maangamizi yatakujia ghaflaambayo hujapata kamwe kuyaona.

12. Endelea basi na uganga wako,tegemea wingi wa uchawi wako.Wewe uliyapania hayo tangu ujana wakoukitumainia kwamba utafanikiwaau kusababisha kitisho kwa watu!

Kusoma sura kamili Isaya 47