Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 44:24-28 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wako,aliyekuumba tangu tumboni mwa mama yako, asema:“Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyeumba vitu vyote.Mimi peke yangu nilizitandaza mbingu,niliiumba dunia kwa nguvu yangu mwenyewe!

25. Mimi huzivuruga ishara za watabiri waongona kuwapumbaza waaguzi.Mimi huyakanusha maneno ya wenye hekimana kufanya ujuzi wao kuwa upumbavu.

26. Lakini huuthibitisha ujumbe wa mtumishi wangu,na kukamilisha maaguzi ya wajumbe wangu.Mimi ndimi niuambiaye mji wa Yerusalemu:Wewe Yerusalemu, utakaliwa tena na watu.Na miji ya Yuda:Nyinyi mtajengeka tena:Magofu yenu nitayarekebisha tena.

27. Mimi ndimi ninayeviamuru vilindi:Kaukeni.

28. Ndimi nimwambiaye Koreshi:Wewe utawachunga watu kwa niaba yangu.Wewe utatekeleza mipango yangu yote.Ndimi ninayesema kuhusu Yerusalemu:Wewe Yerusalemu utajengwa tena upya;na juu ya hekalu: Msingi wako utawekwa tena.”

Kusoma sura kamili Isaya 44