Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 43:15-28 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wenu;Mimi ndimi Muumba wa Israeli, Mfalme wenu.”

16. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wakati mmoja nilifanya barabara baharininikaweka njia kati ya mawimbi makubwa.

17. Nililipiga jeshi lenye nguvu,jeshi la magari na farasi wa vita,askari na mashujaa wa vita.Niliwaangusha chini wasiweze kuinuka tena,niliwakomesha na kuwazima kama utambi wa taa.Sasa nasema:

18. ‘Msiyanganganie mambo yaliyopita,wala msifikirie vitu vya zamani.

19. Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya.Kinafanyika sasa hivi,nanyi mtaweza kukiona.Nitafanya njia nyikani,na kububujisha mito jangwani.

20. Wanyama wa porini wataniheshimu,kina mbweha na kina mbuni,maana nitaweka maji nyikani,na kububujisha mito jangwani,ili kuwanywesha watu wangu wateule,

21. watu niliowaumba kwa ajili yangu mwenyewe,ili wazitangaze sifa zangu!’

22. “Lakini ewe taifa la Yakobo, hukuniabudu mimi;enyi watu wa Israeli, mlinichoka mimi!

23. Hamjaniletea kondoo wenu wa sadaka za kuteketezwa,wala kuniheshimu kwa tambiko zenu.Nami sikuwalemeza kwa kutaka sadaka,wala sikuwachosha kwa kuwadai ubani.

24. Hamkuninunulia manukato kwa faida yenu,wala kuniridhisha kwa nyama nono za tambiko.Badala yake dhambi zenu zimekuwa mzigo kwangu,mmenichosha kabisa kwa makosa yenu.

25. Walakini mimi ndimi niliyefuta makosa yenu kwa heshima yangu,ndimi niyafutaye makosa kwa ajili yangu mwenyewe,na wala sitazikumbuka dhambi zenu.

26. “Niambie kama mna kisa nami,njoo tukahojiane;toeni mashtaka yenu ili tuuone ukweli wenu!

27. Babu yenu wa kwanza alitenda dhambi,wapatanishi wenu waliniasi.

28. Kwa hiyo niliwafanya haramu wakuu wa mahali patakatifunikawaacha watu wa Yakobo waangamizwe,naam, nikawaacha Waisraeli watukanwe.”

Kusoma sura kamili Isaya 43