Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 43:12-23 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Nilitangaza yale ambayo yangetukia,kisha nikaja na kuwakomboa.Hakuna mungu mwingine aliyewahi kufanya hivyo,nanyi ni mashahidi wangu.

13. Mimi ni Mungu na nitakuwa Mungu daima.Hakuna awezaye kuiepa nguvu yangu;hakuna awezaye kupinga ninayofanya.”

14. Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wenu,Mtakatifu wa Israeli, asema hivi:“Kwa ajili yenu nitatuma jeshi Babuloni.Nitayavunjilia mbali malango ya mji wake,na kelele za hao Wakaldayo zitageuka maombolezo.

15. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wenu;Mimi ndimi Muumba wa Israeli, Mfalme wenu.”

16. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wakati mmoja nilifanya barabara baharininikaweka njia kati ya mawimbi makubwa.

17. Nililipiga jeshi lenye nguvu,jeshi la magari na farasi wa vita,askari na mashujaa wa vita.Niliwaangusha chini wasiweze kuinuka tena,niliwakomesha na kuwazima kama utambi wa taa.Sasa nasema:

18. ‘Msiyanganganie mambo yaliyopita,wala msifikirie vitu vya zamani.

19. Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya.Kinafanyika sasa hivi,nanyi mtaweza kukiona.Nitafanya njia nyikani,na kububujisha mito jangwani.

20. Wanyama wa porini wataniheshimu,kina mbweha na kina mbuni,maana nitaweka maji nyikani,na kububujisha mito jangwani,ili kuwanywesha watu wangu wateule,

21. watu niliowaumba kwa ajili yangu mwenyewe,ili wazitangaze sifa zangu!’

22. “Lakini ewe taifa la Yakobo, hukuniabudu mimi;enyi watu wa Israeli, mlinichoka mimi!

23. Hamjaniletea kondoo wenu wa sadaka za kuteketezwa,wala kuniheshimu kwa tambiko zenu.Nami sikuwalemeza kwa kutaka sadaka,wala sikuwachosha kwa kuwadai ubani.

Kusoma sura kamili Isaya 43