Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 40:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mungu wenu asema:“Wafarijini watu wangu,nendeni mkawafariji.

2. Semeni na wenyeji wa Yerusalemu kwa upole,waambieni kwamba utumwa wao umekwisha,wamesamehewa uovu wao.Mwenyezi-Mungu amewaadhibu maradufukwa sababu ya dhambi zao zote.”

3. Sauti ya mtu anaita jangwani:“Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia,nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu.

4. Kila bonde litasawazishwa,kila mlima na kilima vitashushwa;ardhi isiyo sawa itafanywa sawa,mahali pa kuparuza patalainishwa.

5. Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu utafunuliwa,na watu wote pamoja watauona.Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hayo.”

6. Sikiliza! Kuna sauti inasema, “Tangaza!”Nami nikauliza, “Nitangaze nini?”Naye: “Tangaza: Binadamu wote ni kama majani;uthabiti wao ni kama ua la shambani.

7. Majani hunyauka na ua hufifia,Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake.Hakika binadamu ni kama majani.

8. Majani hunyauka na ua hufifia,lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”

Kusoma sura kamili Isaya 40