Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 38:7-19 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Isaya akamjibu, “Hii itakuwa ishara kwako kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwamba Mwenyezi-Mungu atafanya kama alivyoahidi.

8. Nitafanya kivuli kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi, kirudi nyuma hatua kumi.” Nacho kivuli kikarudi nyuma hatua kumi.

9. Kisha mfalme Hezekia alipopona, akatunga wimbo huu wa shukrani:

10. “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa,inanibidi niage dunia.Mimi nimepangiwa kwenda kuzimusiku zote zilizonibakia.

11. Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu,katika nchi ya walio hai;wala sitamwona mtu yeyote tena,miongoni mwa wakazi wa ulimwengu.

12. Makao yangu yamengolewa kwangu,kama hema la mchungaji;kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu;Mungu amenikatilia mbali;kabla hata mwisho wa siku amenikomesha.

13. Usiku kucha nililia kuomba msaada;kama simba, anavunjavunja mifupa yangu;mchana na usiku ananikomesha.

14. “Ninalia kama mbayuwayu,nasononeka kama njiwa.Macho yangu yamefifia kwa kuangalia juu.Ee Bwana, nateseka;uwe wewe usalama wangu!

15. Lakini niseme nini:Yeye mwenyewe aliniambia,naye mwenyewe ametenda hayo.Usingizi wangu wote umenitorokakwa sababu ya uchungu moyoni mwangu.

16. “Ee Bwana, Sisi twaishi kutokana na yote uliyotenda,kwa hayo yote mimi binafsi pia ninaishi.Nirudishie afya, uniwezeshe kuishi.

17. Nilipata mateso makali kwa faida yangu;lakini umeyaokoa maisha yangukutoka shimo la uharibifu,maana umezitupa dhambi zangu nyuma yako.

18. Huko kuzimu mtu hawezi kukushukuru wewe;waliokufa hawawezi kukushukuru wewe.Wala washukao huko shimonihawawezi tena kutumainia uaminifu wako.

19. Walio hai ndio wanaokushukuru,kama na mimi ninavyofanya leo.Kina baba huwajulisha watoto wao uaminifu wako.

Kusoma sura kamili Isaya 38