Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 34:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Karibieni mkasikilize enyi mataifa,tegeni sikio enyi watu.Sikiliza ee dunia na vyote vilivyomo,ulimwengu na vyote vitokavyo humo!

2. Mwenyezi-Mungu ameyakasirikia mataifa yote,ameghadhabika dhidi ya majeshi yao yote.Ameyapangia mwisho wao,ameyatoa yaangamizwe.

3. Maiti zao zitatupwa nje;harufu ya maiti zao itasambaa;milima itatiririka damu yao.

4. Jeshi lote la angani litaharibika,anga zitakunjamana kama karatasi.Jeshi lake lote litanyauka,kama majani ya mzabibu yanyaukavyo,naam, kama tunda la mtini linyaukavyo.

Kusoma sura kamili Isaya 34