Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 33:14-24 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Wenye dhambi katika Siyoni wanaogopa,wasiomcha Mungu wanatetemeka na kusema:“Nani awezaye kuukaribia moto huu mkali?Nani awezaye kustahimili miali ya moto wa milele?”

15. Ni mtu aishiye kwa uadilifu na asemaye ukweli;mtu anayedharau kabisa utajiri wa dhuluma,anayekataa hongo kata kata,asiyekubali kamwe kusikia mipango ya mauaji,wala hakubali macho yake yaone maovu.

16. Mtu wa namna hiyo anaishi juu,mahali salama penye ngome na miamba;chakula chake atapewa daima,na maji yake ya kunywa hayatakosekana.

17. Mtaweza kumwona mfalme katika fahari yake,mtaiona nchi anayotawala, kubwa na pana.

18. Mtafikiria tisho lililopita na kujiuliza,“Wako wapi wale waliokadiria na kukisia kodi?Wako wapi wale waliopeleleza ulinzi wetu?”

19. Hamtawaona tena watu wale wenye kiburi,wanaozungumza lugha isiyoeleweka.

20. Tazameni Siyoni tunamofanya sikukuu zetu;tazameni mji Yerusalemu, makao matulivu, hema imara;vigingi vyake havitangolewa kamwe,kamba zake hazitakatwa hata moja.

21. Humo Mwenyezi-Mungu atatuonesha ukuu wake.Kutakuwa na mito mikubwa na vijito,ambamo meli za vita hazitapita,wala meli kubwa kuingia.

22. Maana Mwenyezi-Mungu ni hakimu wetu,yeye ni mtawala wetu;Mwenyezi-Mungu ni mfalme wetu,yeye ndiye anayetuokoa.

23. Ewe Siyoni, kamba zako zimelegea,haziwezi kushikilia matanga yake,wala kuyatandaza.Lakini nyara nyingi zitagawanywa;hata vilema wataweza kuchukua sehemu yao.

24. Hakuna atakayesema tena ni mgonjwa;watu watasamehewa uovu wao wote.

Kusoma sura kamili Isaya 33