Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 30:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Kauli ya Mungu juu ya wanyama wa pande za Negebu:“Wajumbe wanapita katika nchi ya taabu na shida,yenye simba, nyoka wa sumu na majoka.Wamewabebesha wanyama wao mali zao,kuwapelekea watu wasioweza kuwafaa kitu.

7. Maana msaada wa Misri ni bure, haufai kitu;kwa hiyo nimeipanga Misri jina:‘Joka lisilo na nguvu!’”

8. Mungu aliniambia:“Sasa chukua kibao cha kuandikia,uandike jambo hili mbele yao,liwe ushahidi wa milele:

9. Watu hawa ni waasi, watoto wasioaminika;watu wasiopenda kusikia mafunzo ya Mwenyezi-Mungu.

10. Huwaambia waonaji: ‘Msione maono’,na manabii: ‘Msitutangazie ukweli,bali tuambieni mambo ya kupendeza,toeni unabii wa mambo ya udanganyifu tu.

11. Geukeni na kuiacha njia ya ukweli;msituambie tena juu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli.’”

12. Kwa hiyo Mungu, Mtakatifu wa Israeli asema:“Nyinyi mmeukataa ujumbe wangu;mkapania kufanya dhuluma na udanganyifu.

Kusoma sura kamili Isaya 30