Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 30:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Ole wao watoto wanaoniasi,wanaotekeleza mipango yao na si mipango yangu,wanaofanya mikataba kinyume cha matakwa yangu!Naam, wanarundika dhambi juu ya dhambi.

2. Bila kunitaka shauri, wanafunga safari kwenda Misri,kukimbilia usalama katika ulinzi wa Farao,kupata mahali pa usalama nchini Misri.

3. Lakini ulinzi wa Farao utakuwa aibu yenu,na usalama nchini Misri utakuwa fedheha yenu.

4. Maana ingawa maofisa wao wamefika Soani,na wajumbe wao mpaka Hanesi,

5. wote wataaibishwa na hao wasioweza kuwasaidia,watu ambao hawawezi kuwapa msaada au faida,ila tu kuwapa aibu na fedheha.”

6. Kauli ya Mungu juu ya wanyama wa pande za Negebu:“Wajumbe wanapita katika nchi ya taabu na shida,yenye simba, nyoka wa sumu na majoka.Wamewabebesha wanyama wao mali zao,kuwapelekea watu wasioweza kuwafaa kitu.

Kusoma sura kamili Isaya 30