Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 27:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu atautwaa upanga wake mkubwa, mkali na imara, na kuliadhibu dude Lewiyathani joka lirukalo na danganyifu; Mwenyezi-Mungu ataliua joka liishilo baharini.

2. Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu atasema hivi:“Imbeni utenzi wa shamba langu zuri la mizabibu!

3. Mimi, Mwenyezi-Mungu, ni mkulima wake;nalimwagilia maji kila wakati,ninalilinda usiku na mchana,lisije likaharibiwa na mtu yeyote.

4. Silikasirikii tena shamba hili;kama miiba na mbigili ingelilivamia,mimi ningepambana nayo na kuichoma moto.

5. Maadui za watu wangu wakitaka ulinzi wangu,basi, na wafanye amani nami;naam, wafanye amani nami.”

6. Itakuja siku wazawa wa Yakobo watashika mizizi;naam, watu wa Israeli watachanua na kuchipua,na kuijaza dunia yote kwa matunda.

Kusoma sura kamili Isaya 27