Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 24:9-21 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Hakuna tena kunywa divai na kuimba;mvinyo umekuwa mchungu kwa wanywaji.

10. Mji uliohamwa umejaa uharibifu;kila nyumba imefungwa asiingie mtu.

11. Kuna kilio barabarani kwa kukosa divai;shangwe yote imekoma,furaha imetoweka duniani.

12. Mji ni magofu matupu;malango yake yamevunjwavunjwa.

13. Kama vile zeituni chache tu juu ya mzeituniau tini chache tu juu ya mtinibaada ya kumaliza mavuno,ndivyo itakavyokuwa katika nchi zote:Watu wachache watabakia hai.

14. Watakaosalia watapaza sauti,wataimba kwa shangwe.Kutoka magharibi watatangaza ukuu wa Mwenyezi-Mungu,

15. nao wakazi wa mashariki watamsifu.Watu wa mbali watalisifujina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.

16. Tunasikia nyimbo za sifa kutoka miisho ya dunia,nyimbo za kumsifu Mungu aliye mwadilifu.Lakini mimi ninanyongonyea,naam, ninanyongonyea.Ole wangu mimi!Wasaliti wanaendelea kuwa wasaliti,usaliti wao unazidi kuwa mbaya zaidi.

17. Hofu, mashimo na mitego,hivi ndivyo vinavyowangojeni enyi wakazi wa dunia.

18. Atakayeikimbia hofu atatumbukia shimoni;atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni.Madirisha ya mbinguni yamefunguliwa,misingi ya dunia inatikisika.

19. Dunia inavunjikavunjika,inapasuka na kutikiswatikiswa.

20. Inapepesuka kama mlevi,inayumbayumba kama kibanda.Imelemewa na mzigo wa dhambi zakenayo itaanguka wala haitainuka tena.

21. Siku ile Mwenyezi-Mungu ataliadhibu jeshi la anganikadhalika na wafalme wa duniani.

Kusoma sura kamili Isaya 24