Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 24:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sasa Mwenyezi-Mungu anaiharibu duniana kuifanya tupu.Atausokota uso wa duniana kuwatawanya wakazi wake.

2. Kila mtu atapatwa na mambo yaleyale:Mtu wa kawaida na kuhani;mtumwa na bwana wake;mjakazi na bibi yake;mnunuzi na mwuzaji;mkopeshaji na mkopaji;mdai na mdaiwa.

3. Dunia itaharibiwa kabisa na kuangamizwa;Mwenyezi-Mungu ametamka hayo.

4. Dunia inakauka na kunyauka;ulimwengu unafadhaika na kunyauka;mbingu zinafadhaika pamoja na dunia.

5. Watu wameitia najisi duniamaana wamezivunja sheria za Mungu,wamezikiuka kanuni zake,wamelivunja agano lake la milele.

6. Kwa sababu hiyo laana inaitokomeza dunia,wakazi wake wanateseka kwa makosa yao.Wakazi wa dunia wamepungua,ni watu wachache tu waliosalia.

7. Mizabibu inanyauka,divai inakosekana.Wote waliokuwa wenye furahasasa wanasononeka kwa huzuni.

Kusoma sura kamili Isaya 24