Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 24:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sasa Mwenyezi-Mungu anaiharibu duniana kuifanya tupu.Atausokota uso wa duniana kuwatawanya wakazi wake.

2. Kila mtu atapatwa na mambo yaleyale:Mtu wa kawaida na kuhani;mtumwa na bwana wake;mjakazi na bibi yake;mnunuzi na mwuzaji;mkopeshaji na mkopaji;mdai na mdaiwa.

3. Dunia itaharibiwa kabisa na kuangamizwa;Mwenyezi-Mungu ametamka hayo.

4. Dunia inakauka na kunyauka;ulimwengu unafadhaika na kunyauka;mbingu zinafadhaika pamoja na dunia.

5. Watu wameitia najisi duniamaana wamezivunja sheria za Mungu,wamezikiuka kanuni zake,wamelivunja agano lake la milele.

Kusoma sura kamili Isaya 24