Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 23:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kauli ya Mungu dhidi ya Tiro.Ombolezeni, enyi mabaharia wa mbali baharini,maana Tiro mji wenu umeharibiwa,humo hamna tena makao wala bandari.Mtazipokea habari hizo mtakaporejea kutoka Kupro.

2. Nyamazeni kwa mshangao enyi wakazi wa pwani,naam, tulieni enyi wafanyabiashara wa Sidoni,ambao wajumbe wenu wanapita baharini,

3. wakasafiri katika bahari nyingi.Mapato yenu yalikuwa nafaka ya Misri,mkaweza kufanya biashara na mataifa.

4. Aibu kwako ewe Sidoni,mji wa ngome kando ya bahari!Bahari yenyewe yatangaza:“Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa,wala sijawahi kuzaa;sijawahi kulea wavulana,wala kutunza wasichana!”

5. Habari zitakapoifikia Misrikwamba Tiro imeangamizwa,Wamisri watafadhaika sana.

Kusoma sura kamili Isaya 23