Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 2:19-22 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Ingieni katika mapango miambani,katika mashimo ardhini,kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu,mbali na utukufu wa enzi yake,atakapokuja kuitia hofu dunia.

20. Siku hiyo, watu watawatupia panya na popovinyago vyao vya fedha na dhahabuwalivyojitengenezea ili kuviabudu.

21. Nao wataingia katika mapango miambanina kwenye nyufa za miamba,kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu,mbali na utukufu wa enzi yake,atakapokuja kuitia hofu dunia.

22. Usimwamini binadamu,uhai wake haudumu kama pumzi.Yeye anafaa kitu gani?

Kusoma sura kamili Isaya 2