Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 2:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno alilopewa Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na Yerusalemu.

2. Siku zijazo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Munguutaimarishwa kupita milima yote,utainuliwa juu ya vilima vyote.Mataifa yote yatamiminika huko,

3. watu wengi wataujia na kusema,“Njoni tupande mlima wa Mwenyezi-Mungu,twende nyumbani kwa Mungu wa Yakobo,apate kutufundisha njia zake,nasi tuishi kadiri ya mwongozo wake.Maana sheria itakuja kutoka Siyoni;neno la Mwenyezi-Mungu kutoka Yerusalemu.”

4. Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifaatakata mashauri ya watu wengi.Watu watafua panga za vita kuwa majembena mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea.Taifa halitapigana na taifa linginewala hayatafanya tena mazoezi ya vita.

5. Sasa, enyi wazawa wa Yakobo, njoni,tutembee katika mwanga wa Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Isaya 2