Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 16:7-14 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Sasa Wamoabu wanalia;wote wanaomboleza juu ya nchi yao.Ombolezeni kwa pigo hilo kubwa,na juu ya maandazi ya zabibu za Kir-haresethi.

8. Mashamba ya Heshboni yamefifia.Kadhalika na zabibu za Sibmaambazo ziliwalevya wakuu wa mataifazikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani,chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.

9. Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazerikwa ajili ya mizabibu ya Sibma.Machozi yananitoka kwa ajili yenu,enyi miji ya Heshboni na Eleale;maana vigelegele vya mavuno ya matunda,vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka.

10. Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba la rutuba.Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena,wala kupiga vigelegele.Hakuna tena kukamua zabibu shinikizoni,sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.

11. Hivyo, nafsi yangu yalilia Moabu kama kinubi,na moyo wangu kwa ajili ya mji wa Kir-heresi.

12. Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao,wanapojichosha huko juu mahali pa ibada,wanapokwenda mahali pao patakatifu kusali,hawatakubaliwa.

13. Hili ndilo jambo alilosema Mwenyezi-Mungu wakati uliopita kuhusu Moabu.

14. Lakini sasa Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Baada ya miaka mitatu kamili, ikihesabiwa kama mfanyakazi anavyohesabu siku zake, fahari ya Moabu itakwisha. Ingawa watu wake ni wengi, watakaobaki hai watakuwa wachache na wanyonge.”

Kusoma sura kamili Isaya 16