Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 14:26-32 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Huu ndio uamuzi wake Mwenyezi-Mungukuhusu dunia yote;hii ndiyo adhabu atakayotoajuu ya mataifa yote.

27. Kama Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameamua,nani atakayeweza kubatilisha uamuzi wake?Kama amepania kutoa adhabu,ni nani atakayempinga?

28. Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii:

29. “Msishangilie enyi Wafilisti wote,kwamba Ashuru, fimbo iliyowapiga, imevunjika;maana, nyoka wa kawaida atazaa nyoka mwenye sumu,na nyoka mwenye sumu atazaa joka lirukalo.

30. Wazaliwa wa kwanza wa maskini watashiba,na fukara watakaa kwa usalama.Lakini chipukizi wenu nitawaua kwa njaa;na yeyote wenu atakayebaki nitamuua.

31. Piga yowe ewe lango; lia ewe mji;yeyuka kwa hofu ewe nchi yote ya Filistia.Maana moshi wa askari waja kutoka kaskazini,wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake.”

32. Basi watapewa jibu gani wajumbe wa taifa hilo?Wataambiwa: Mwenyezi-Mungu ameijenga imara Siyoni,na maskini wa watu wake watakimbilia usalama huko.

Kusoma sura kamili Isaya 14